Dkt. Magufuli ataka Watanzania wachape kazi badala ya kupiga makelele

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewataka watanzania kuchapa kazi badala ya kupigia kelele suala la mabadiliko ya katiba katika mitandao ya kijamii  nakueleza kua suala hilo litafuatwa kwa wakati wake ukifika

Akizungumza wakati wa kuchangia kwenye kongamano la kujadili hali ya uchumi na siasa katika kipindi cha miaka mitatu ya utawala wake, Rais Magufuli amesema kuwa hategemei kutenga fedha kwa sasa kwa ajili ya kurejesha mchakato wa Katiba mpya.

Nafahamu hamu ya watanzania kuwa na katiba mpya, sasa tunafanyaje!? Tunaendelea na hii rasimu pendekezwa au tunaenda kwenye ile ya kwanza iliyofanywa na Jaji Warioba!? Sasa badala ya kuanza kujibizana na haya ngoja tuchape kazi“, amesema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli amebainisha kuwa anakutana na changamoto pindi anapofanya uteuzi mbalimbali hasa kwa wanawake ikiwemo madai anayopelekewa ambayo hayana ukweli na kuahidi kuendelea kuwapa nafasi kwenye uongozi wake

Kwa mujibu wa Rais Magufuli wakati akifanya uteuzi wa wanawake amekuwa akituhumiwa kuteua watu ambao ana mahusiano nao mbali na mahusiano ya kikazi.

Nimeteua kina mama wengi, na sasa hivi kila unayemteua kina mama ni hawara yako, na nitaendelea kuwateua tu, kuna wakati wanaofanya hivi ni kina mama wenyewe, sijui wanataka niteue wanaume tu, mimi nitaendelea kuwateua“, amesema Rais Magufuli.