Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein leo amekutana na Uongozi wa benki ya CRDB Ikulu Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar.

Rais Dkt Shein katika mazungumzo yake amesisitiza haja kwa Benki ya CRDB kuendelea kutoa huduma zake kwa pande zote mbili za  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili wananchi  wote wafaidike na matunda ya benki hiyo.


Dk. Shein aliyasema hayo leo, Ikulu Jijini Zanzibar wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki ya CRDB Abdulmajid Mussa Nsekela aliyefika Ikulu kwa ajili ya kujitambulisha akiwa amefuatana na uongozi wa Benki hiyo ulioongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Ally Hussein Laay.