Kampuni ya kutengeneza ndege ya Boeing imetangaza kwamba itatoa Dola Milioni 100 kwa familia, Serikali na Mashirika yasiyo ya kiserikali ya Ethiopia na Indonesia ili kusaidia familia za watu waliopoteza maisha kwenye ajali mbili za ndege muundo wa 737 MAX.

Kwa mujibu wa Reuters, hatua hiyo ni katika juhudi za kuimarisha taswira ya kampuni hiyo ambayo hadhi yake imeshuka kwa kiwango kikubwa katika siku za karibuni.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Dennis Mullenburgh, amesema kuwa pesa hizo zitatolewa kwa kipindi cha miaka kadhaa ijayo ingawa hakutoa utaratibu utakaofuatwa.