Wananchi wametakiwa kuwa na muamko wa kulipa kodi na kuiyunga mkono serikali yao kila inapoanzisha kodi mpya ili kutatua changamoto nchini

Wito huo umetolewa na rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr Ali Mohd Shein ambae pia ni mgeni rasmini katika maadhimisho ya miaka 20 toka kuanzishwa bodi ya mapato (ZRB) halfa iliyofanyika katika afisi zao huko mzizini mjini unguja

Dr shein amesema kulipa kodi ni wajibu wa kila mwanachi na maendeleo mengi yametokana na kodi za wananchi wa Zanzibar hivyo kila mwananchi anawajibu wa kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi

Aidha Dr Shein amesema Serikali imepunguza utegemezi kwa asilimia kubwa yote hii kutokana na mapato yanayokusanywa pamoj na kutoa zawadi kwa skuli ya fidelkasro pemba na bembela kwa unguja kwa madahalo wa juu ya umuhimu wa kulipa kodi

Naye kamishna wa bodi ya mapato Zanzibar (ZRB) Joseph Abdallah Meza ametoa changamoto zinazowakabili katika bodi yao ambapo amesema kuwa baadhi ya wafanya biashara kutokulipa kodi kwa wakati hali inayopelekea usumbufu wa watendaji wa bodi hiyo

Bodi ya mapato zanzibar (ZRB) imetimiza miaka 20 toka kuanzishwa kwake ambapo mpaka sasa inaendelea kukusanya kodi ambayo hutumika katika maendeleo ya zanzibar