Msanii maarufu ambae pia ni msanii mkongwe wa Bongo Fleva, Dudu Baya amesema kuwa adhabu aliyopanga kumpatia msanii Harmorapa ipo pale pale.

Inakumbukwa mara baada ya Harmorapa kuingilia kati kitu ambacho Dudu Baya alikiita ni vita dhidi ya ushoga, Dudu Baya alihahidi kumpatia kichapo msanii huyo mwenye matukio ya aina yake kwenye muziki.

Dudu Baya amekuwa akihusishwa kugombana na wasanii mbalimbali akiwemo Mr. Nice aliyempiga na muumiza vibaya kitu kilichopelekea Dudu Baya kushikiliwa gerezani.

“Hakuna nilichobadilisha, adhabu yako ipo pale pale,” amesisitiza Dudu Baya ambaye kwa sasa
anatamba na wimbo Koki aliyomshirikisha Rayvanny.