Edo akatishwa tamaa na timu ya Mafunzo ‘Ni vigumu kuendelea na timu hii’

Kocha msaidizi wa klabu ya Mafunzo ambaye pia ni mchezaji wa Zamani wa klabu hiyo Abdalla Bakar (Edo) amesikitishwa na klabu yake kufanya vibaya kwenye ligi kuu ya Zanzibar msimu huu.

Akizugumza na Zanzibar24 baada ya kumalizika mchezo wao dhidi ya Hardrock jana ambapo Mafunzo wamepoteza mchezo huo amesema wamejifunza mengi ndani ya ligi hiyo licha ya kufuzu kwenye hatua ya nane bora.

Kuhusu hali ya timu amesema amesikitishwa sana kuona ushindani mdogo sana ndani ya Mafunzo na wachezaji wake wengi tayari wameshakuwa hawawezi kucheza ligi kuu ya Zanzibar kwa umri wao kuwa mkubwa sana.

‘’ Nivigumu kuendelea na timu hii ambayo wachezaji watano muhimu tayari wamekuwa watu wazima siwezi kuwa na timu ya ushindani wa kucheza ligi kuu ya Zanzibar msimu unao kuja’’ Alisema kocha Edo.

Mafunzo imemaliza ligi kuu ya Zanzibar ikiwa na alama 15 wakiwa nafasi ya tano ya msimamo wa ligi kuu ya Zanzibar hatua ya nane bora ,katika hatua ya kanda ya ligi kuu ya Zanzibar Mafunzo ilikuwa ikinolewa na Hemedi Suleiman Moroko.