Diwani wa kata ya Ngokolo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Manispaa ya Shinyanga, Emmanuel Ntobi amefukuzwa kwenye Baraza la Madiwani na kutohudhuria vikao vitatu vya baraza hilo.

Pia diwani huyo atanyimwa stahiki zake zote kwa kipindi hicho alichosimamishwa kutokana na tuhuma za kuichafua manispaa hiyo kupitia mitandao ya kijamii.

Imedaiwa kuwa diwani huyo amekua akiichafua manispaa hiyo mara kwa mara kwenye mitandao kuwa inafanya ufujaji wa fedha kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo.