Mwigizaji maarufu wa Bongo Movie Esha Buheti amenusurika kifo baada ya kupata ajali wakati akiwa safarini, ajali hiyo imesababishwa na ng’ombe aliyekatiza Barabarani .

Esha ameshare video na picha kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuelezea ilivyokuwa mpaka ajali ikatokea licha ya kuwa wote waliokuwa Kwenye gari hilo wametoka wazima licha ya gari yake kuharibika vibaya.

“Asanteni kwa message na simu nyingi sana ila kwa sasa kichwa kinauma sana, ni kweli tumepata ajali ila tumetoka salama” aliandika Esha kupitia ukurasa wake wa Instagram