Esma Khan atoa neno ndoa ya Diamond Platnumz na Tanasha

Kama vipi poa tu! Dada wa staa mkubwa Afro-Pop nje na ndani ya Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Esma Khan amefunguka kuwa kama kaka’ke huyo atachukua uamuzi wa kumuoa mrembo kutoka Kenya, Tanasha Donna, kwake yeye anabariki kwa sababu ni chaguo lake.

 Esma aliliambia Ijumaa kuwa, hadhani kama ni vyema kumchagulia kaka’ke mke, bali macho yake ndiyo yanaona wapi ni bora aangukie hapo na atakapopachagua na kumuonesha atampokea tu.

 “Unajua hata leo Diamond  akimtambulisha rasmi Tanasha kuwa anataka kumuoa, mimi kama dada, nitaona ni jambo la heri kwenye familia yetu ambayo kila kukicha tunamuombea apate mke bora,” amesema

Esma ambaye amekuwa akipewa jina la Yuda mitandaoni kutokana na kuwageuka wapenzi wa kaka’ke huyo.