Mtandao wa kijamii wa Facebook kwa sasa inakumbwa na hali mbaya zaidi ya mawasiliano kuwahi kutokea katika historia yake kwani huduma nyingi hazipatikani kote ulimwenguni.

Haijabainika wazi ni nini kinachosababisha shida hiyo. Tunafanya kila juhudi kushughulikia tatizo lililopo haraka iwezekanavyo.”

“Tunafahamu kuwa baadhi ya watu hawana hawawezi kufikia app zinazohusiana na Facebook ,” ilisema taarifa iliyotolewa na Facebook.

Kando na Facebook yenyewe, huduma za Messenger na Instagram zimetatizwa.

Mara ya mwisho Facebook ilijipata katika hali hiyo ilikuwa mwaka 2008 wakati mtandao huo ulikuwa na watumiaji milioni 150 -ikilinganishwa na sasa ambapo watumiaji karibu wanakadiriwa kuwa karibu bilioni 2.3 kwa mwezi.

Kampuni ya Facebook imejibu uvumi unaoendelea mitandaoni kuwa huenda mtandao huo maarufu duniani umedukuliwa. Inasema hali hiyo haijatokana na shambulio lolote la kimtandao