Fahamu faida 10 za kupumzika

Unajua kuwa kupumzika huepusha ajali za barabarani

Ni wazi kuwa watu wengi hawafahamu umuhimu wa kupumzika, ndiyo maana hawatengi muda wa kutosha wa kupumzika. Ni ukweli usiopingika kuwa kupumzika kuna manufaa makubwa sana kwenye miili na utendaji wetu wa kazi kila siku.

Ikiwa unataka kuboresha utendaji wako wa kazi pamoja na afya yako, fahamu faida 10 za kupumzika.

1. Huongeza uwezo wa kumbukumbu
Utafiti uliofanyika umebaini kuwa kutokupumzika huongeza kiasi fulani cha protini kwenye ubongo ambacho huchangia katika kutokea kwa maradhi ya Alzheimer (Ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu).

2. Huondoa hatari ya kupata kiharusi
Utafiti uliofanyika umebaini kuwa uchovu hasa ule unaoambatana na msongo wa mawazo, unaweza kusababisha kupasuka kwa mishipa inayopeleka damu kwenye ubongo na kisha kusababisha ugonjwa wa kiharusi.

3. Hulinda afya ya moyo
Kupumzika kuna manufaa makubwa kwenye afya ya moyo wako, Uapopata muda wa kupumzika unaupa moyo wako nafasi ya kupunguziwa mzigo wa kusukuma damu kwa kasi, ambao umeubeba wakati ulipokuwa unafanya shughuli mbalimbali.

4. Hutoa muda wa mwili kujijenga
Miili yetu inahitaji kujijenga kila mara hasa baada ya shughuli nyingi. Kwa njia ya kupumzika utaweza kuupa mwili wako nafasi nzuri ya kujijenga na kurejeshha tena nguvu iliyotumika wakati wa shughuli mbalimbali.

5. Huongeza hamasa ya utendaji
Kupata muda wa kutosha wa kupumzika kutakuwezesha kujisikia vizuri na kuwa tayari kutekeleza majukumu yako kwa ufanisi mkubwa.

6. Huimarisha misuli
Tunapopumzika misuli yetu inajijenga na kurudisha ute wake uliopotea wakati wa shughuli mbalimbali. Hivyo ni muhimu kuhakikisha kila baada ya kazi tunapata muda wa kutosha wa kupumzika ili tuboreshe afya za miili yetu.

7. Huimarisha kinga mwili
Kinga mwili ni muhimu sana kwani hutuwezesha kukabiliana na magonjwa. Kwa njia ya kupata muda wa kutosha wa kupumzika tunatoa nafasi kwa mfumo mzima wa kinga mwili kujijenga na kujiimarisha.

8. Huondoa msongo wa mawazo
Chanzo kimojawapo cha msongo wa mawazo ni uchovu, na chanzo kimojawapo cha maradhi mbalimbali ni msongo wa mawazo.

Hivyo ni muhimu kuhakikisha tunapumzika ili akili na fikra zetu zijisafishe na kutuepusha na tatizo la msongo wa mawazo.

10. Huepusha ajali za barabarani

Je ulishasikia ajali zilizosababishwa na madereva wanaosinzia? Uchoovu na kukosa muda wa kupumzika (hasa kulala) humfanya mtu akose utulivu na uwezo wa kumudu chombo anachoedesha.

Hivyo ni muhimu kwa madereva na watu wote wanaotumia vyombo vya usafiri kuhakikisha wanapata muda mzuri na wakutosha wa kupumzika.