Ni watu wachache sana ndiyo wanaopenda na wanafahamu umuhimu wa kusoma vitabu. Watu wengi hasa waafrika hawapendi kusoma vitabu ikiwa hakuna kinachowalazimisha kufanya hivyo kama vile mtihani, kazi, n.k.

Kwa hakika kuna maarifa mengi yaliyofichwa kwenye vitabu; hii ndiyo sababu watu wengi waliofanikiwa husoma au hata kuandika vitabu.

Ikiwa unataka kupata maarifa na kuboresha maisha yako kwa njia ya kusoma vitabu, basi fahamu faida za kusoma vitabu.

  1. Njia za kukabiliana na matatizo mbalimbali.
  2. Njia za kufanya mambo mbalimbali kwa ufanisi.
  3. Jinsi ya kuboresha maisha yako.
  4. Hamasa kutoka kwa waliofanikiwa n.k.
  5. Maarifa mapya usiyoyajua.

Haya ni baadhi tu ya mambo ambayo unaweza kujifunza au kuyapata kutoka kwenye vitabu. Hivyo ikiwa unataka kuwa bora zaidi jizoeze kusoma vitabu mbalimbali kila mara.