Fereji aitaka Serikali kuisadia ZFA

Mwanamichezo mkongwe wa mpira wa miguu Zanzibar, pia aliwahi kuwa Raisi wa chama cha mpira wa miguu Zanzibar (ZFA) Ali Fereji Tamimu ameitaka serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kuisadia ZFA kuundeleza  mpira wa Zanzibar.

Akizugumza na Zanzibar24 nyumbani kwake Ali Fereji amesema licha ya ZFA kuwa ni chama huru kuendesha mchezo wa mpira wa miguu Zanzibar lakini kina hitaji sana msaada wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Aidha Ali Fereji amesema wakati akiongoza yeye ZFA alifanikiwa sana kwa kuwa alishirikiana vizuri sana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kufanikiwa vizuri ikiwemo timu ya Taifa ya Zanzibar kuchukua ubingwa wa CECAFA  mwaka 1995 na yale mashindano ya vijana ya Senior CECAFA  na kwa kuwa na mipango mizuri ya kuendesha mpira wa Zanzibar.

‘’Serikali ina mchango mkubwa sana kusogeza mpira wa Zanzibar tena namuomba Katibu Mkuu Omar Hassan Omar asaidie soka la Zanzibar yeye alikuwa mchezaji mkubwa na mzuri sana Zanzibar, lazima asaidie tuko vibaya sasa hivi’’ Alisema Fereji.

Kwa upande mwengine Ali fereji Tamimu amesema hakubaliani na kanuni ya kucheza ligi kuu ya Zanzibar kwa mfumo wa kanda ambayo iliyotumika kwa muda mrefu kwa kuwa si mfumo rafiki wa kucheza ligi kuu ya Zanzibar.

Ali Fereji amefunguka kwa kusema wakati wa uongozi wake aliwahi kutafuta mtaalamu wa soka kutoka ujerumani na kutakiwa kuwa na vilabu 12 tu kwenye ligi kuu ya Zanzibar.

‘’sasa hivi kuna vilabu vingi utiriri wa vilabu wakati wangu Mundu ya Nungwi  alichukua ubingwa wa Zanzibar na Jamuhuri ya Pemba ilichukua ubingwa wa Zanzibar sasa hivi ni tabu vilabu hivi kuja juu.’’ Alimalizia  Fereji.