Fid Q baada ya kushambuliwa na mashabiki mtandaoni  ameamua kueleza alichomaanisha kwenye clips ya tangazo la Tigo Fiesta ambalo linasambaa mtandaoni akitafsirikiwa kwamba alitupa dongo kwa Wasafi Festival.

Kupitia video hiyo, Fid alisikika akisema:-

“Yani nyinyi mnataka kusubiri watu wafanye halafu na nyie mfanye, kawambie acheni upumbavu ni moja kubwa” kauli ambayo ilitafsiriwa ni dongo kwa kwambi hiyo.

Rapa huyo kutoka Mwanza Jumanne hii ameamua kutoa kauli yake huku akiomba radhi wa WCB kama walimtafsiri vibaya kwani hakuwa na nia ya kuwarushia vidongo.

PART 1: Nimeonelea si vibaya nikifungua hiki kigazeti changu na sentensi hii—-.> “ Keki ya taifa ni kubwa sana na ina vipande vingi vya kuwatosha wachakarikaji wote wenye kuistahiki “
Na kwakua Allah ndio mtoaji riziki, mimi kama mimi sina hayo mamlaka au hata hiyo roho mbaya ya kutamani wachakarikaji wenzangu mkwame ktk harakati zenu, ninasema hivi ni kwasababu siku zote huwa siamini kama nitapungukiwa kitu nyinyi mkifanikiwa, na siamini hivyo kwasababu ninajiamini mimi ni mchakarikaji na kipande changu cha KEKI bado kipo mezani kinaningojea ( cha muhimu ni PUMZI na DUA tu ).. ni ukweli tupo kwenye tasnia moja na kila mmoja wetu anajaribu kufanya lile alionalo sahihi ili kusogea mbele, na iko wazi mmeshafanya na mnaendelea kufanya mengi makubwa, nami bila kusita siku zote nimekua ni mtu wa kuwapongeza iwe kwa njia ya mitandao au tukutanapo ana kwa ana.. mie hufanya vile kiroho safi pasina chembe yoyote ya unafiki. ••••••••••••
Nimeyasema hayo hapo juu ili tu uweze au muweze kupata picha halisi ya kilichomo moyoni mwangu na pia kuwakumbusha ya kwamba mimi pia ninao uhuru wa kufanya shughuli zangu za sanaa na yeyote ambaye nimeridhia nae kimaslahi pasina kujali kama jicho la pembeni yangu linaiona faida iliyopo au laah.. sioni ni busara kwa nyie kuja na kujaribu kunipangia yupi nifanye nae au yupi nisifanye nae ili kuwaridhisha machoni/ mioyoni mwenu.. na kama mnaamini ni haki yenu ya msingi mimi kuyafuata hayo matakwa yenu basi naomba nikujuzeni ndugu zangu mtakua mmeonyesha UBINAFSI wa hali ya juu kwenye hili.. pia kumbukeni mimi pia nishawahi kuwa na matatizo na MJENGO.. lakini nilijikuta ninapambana peke yangu hadi UTULIVU uliporejea pasina msaada wa mtu yeyote.. na sikupambana peke yangu kwasababu hamkua na taarifa, taarifa mlikua nazo lakini ninafikiri mlikua mmetingwa na shughuli zenu za ujenzi wa taifa kiasi kwamba hamkuona kama kuniongezea nguvu ingesaidia lile zoezi kuisha haraka.. amini msiamini sijawahi kumuwekea mtu yeyote kinyongo kwenye hilo, na hiyo kitu ilinifunza sana juu ya suala zima la KUJIPAMBANIA MIE MWENYEWE kwenye situation yoyote ile na KUTOKUPIGANA VITA NISIYOIJUA au ISIYONIHUSU.

PART 2: Yote na yote.. Kiukweli yale maneno ya kwenye promo ya “MOJA KUBWA” sikutegemea kama yangekua na uzito huu uliopelekea ndugu yangu uchafukwe kiasi cha kunifungulia bomba la matusi humu insta.. kwanza sikumbuki hata kama niliyatamka kwa nia ya kuleta msigishano huu.. Lakini kama kweli nimewakwaza… Naomba mnisamehe kibinadamu kwa hilo ,naomba tumuache SHETANI apite na mwisho naomba nimalize kwa kusema.. BURUDANI sio VITA <hivyo ninawatakia kila la heri/ MAFANIKIO ya hali ya juu ktk MAPINDUZI YA BURUDANI huko MTWARA.. KEKI YA TAIFA NI KUBWA SANA NA INA VIPANDE VINGI VINAVYOTOSHA KUMFIKIA KILA ANAYESTAHIKI KWA KUDRA ZAKE MUWEZA WA VYOTE…. MAULID NJEMA 🙏🏾