Msimu Jafari Elewi mwenye umri wa miaka 25 mkaazi wa Kitumba anatuhumiwa kuchoma moto gari aina ya Spacio yenye Rangi ya Blue Light huko Kitumba Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.

Akithibitisha kuchomwa kwa moto kwa gari hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Kamanda  Suleiman Hassan Suleiman amesema tukio hilo limetokea siku ya jumamosi ya tarehe 7-03-2020 majira ya 9:00 Usiku huko Kitumba .

Amesema kuwa gari hio ni ya ndugu Abdalla Hiji Abdalla mwenye umri wa miaka 45 Mkaazi wa Kitumba.

Aidha Kamanda Suleiman amesema chanzo cha awali inadaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi .

Rauhiya Mussa