Giza lasababisha mechi dhidi ya Malindi na Polisi Zanzibar kusitishwa

Giza Lapelekea kuhairishwa kwa mchezo wa nusu Fainali ya FA CUP baina ya klabu ya Malindi na Polisi Zanzibar ,mchezo huo ulionza kuchezwa majira ya saa kumi za jioni  Uwanja wa Amani Mjini Unguja nusu fainali ya kwanza ya kombe la FA Cup Zanzibar .

Kipindi cha kwanza mchezo huo licha ya timu zote kushambuliana lakini hakuna timu iliyoona lango la mwenziwe licha ya klabu ya Malindi kulishambulia lango la klabu ya polisi lakini bila ya kuzaa matunda,kipindi cha pili cha mchezo huo timu hizo zilingia kwa kasi lakini hakuna aliyeweza kuzalisha goli.

Baada ya mwamuzi wa mchezo Edi kupuliza kipenga cha mwisho dakika 90 ,kwa mujibu wa kanuni ya michezo hiyo mchezo huo uliongezwa dakika 30 za nyongeza kwa kila kipindi dakika 15 na ilipogonga majira ya saa 12 za jioni kukawa hakuna taa katika uwanja wa Amani Mjini Unguja.

Baada ya kukamilika kipindi cha kwanza cha dakika 15 za nyongeza timu zilibadilishana magoli baada ya muda mfupi kiza kikaanza kutanda kwenye uwanja wa Amani huku hakuna dalili ya kuwashwa taa hizo za Uwanja wa Amani, licha ya mchezo huo kuwa unavutia kwa ushindani katika robo ya kipindi cha pili mwamuzi Edi aliuvunja mchezo huo na matokeo ya kiwa sare bila ya kufungana.

Baadhi ya mashabiki kiwanjani hapo wameshusha lawama kwa kusema ni aibu kwa uwanja mkubwa kama wa Amani unaotumika kucheza mashindano ya kimataifa kuharibika kwa taa za uwanja huo bila ya kufanyiwa marekibisho kwa haraka.

Wengine waliitaka serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kupitia wizara husika kuiondoa aibu ile ambayo inaweza kutia doa sekta ya michezo Zanzibar na kwa sasa dunia inakoelekea michezo ya usiku ndiyo inayoangaliwa zaidi duniani.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kamati ya ZFA mchezo huo utarejewa leo majira ya saa tisa za jioni uwanja wa Amani .

Majira ya saa kumi za jioni nusu fainali ya pili itakutanisha baina ya KMKM dhidi ya Raskazone ,wakati  kisiwani Pemba Jamuhuri amefuzu fainali ya mashindano hayo atacheza dhidi ya Dogo Moro kusubiri mchezo wa mwisho wa Fainali baina ya Bingwa wa Unguja na Pemba.