Kumekuwa na msisimko mkubwa miongoni mwa Wakenya katika mitandao ya kijamii kufuatia hatua ya Google kumuenzi mwandishi maarufu wa fasihi nchini humo.

Margaret Atieno Ogola amekumbukwa leo, siku ambayo angelikuwa hai angekuwa anatimiza miaka 60 tangu kuzaliwa kwake

Alipata umaarufu mkubwa kwa kitabu chake cha kwanza kilichosomwa na wengi nchini, ‘The River and the Source’, ambacho kilijishindia tuzo ya fasihi ya Jomo Kenyatta mnamo 1995 na pia zawadi kwa kitabu cha kwanza bora ya tuzo ya waandishi wa Jumuiya ya madola.

Kitabu hicho kilichotumika katika mtaala wa shule za upili katika miaka ya 90 kinaangazia maisha ya vizazi tofuati vya wanawake nchini Kenya tangu vijijini mpaka katika maisha ya kileo mjini Nairobi.

Chanzo: BBC Swahili.