Mvua inayoendelea kunyesha kwa siku mbili mfululizo imesababisha mafuriko makubwa katika maeneo mbalimbali Jijini Dar es Salaam, ikiwemo eneo la Jangwani ambapo maji yamefunga barabara ya Morogoro, Hakuna gari inayokwenda wala kurudi mjini.
Mwili wa mtu mmoja mwenye jinsia ya kiume umeripotiwa kuokotwa katika mto kenge uliopo Tabata jijini humo.
Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema amefika katika eneo hilo nakuwataka wananchi kuondoka katika maeneo hayo kwasasa kwakuwa maji yanaendelea kuongezeka.
Mbunge wa Ilala Musa Zungu amefika na kueleza kuwa mafuriko hayo ni makubwa ingawa mpaka sasa hawajapata takwimu sahihi ya uharibifu unaotokana na mafuriko hayo.