Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Ndg Ali Mohamed Shein akiwasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba Jijini Dar es salaam na kupokelewa na Katibu Mkuu Ndg Bashiru Ally (Kulia) kwa ajili ya kuhudhuria kikao cha Kamati Kuu.

Katibu Mkuu Ndg Bashiru Ally akimuongoza Mjumbe wa Kamati Kuu na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg @SuluhuSamia
alipofika ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es salaam kushiriki kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa.

Katibu Mkuu Ndg Bashiru Ally akimpokea Ndg Kassim Majaliwa, Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipowasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu Lumumba mapema leo tarehe 12/2/2020 alipofika kuhudhuria kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa.