anne kilango

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, mchana huu ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mama Anne Kilango Malecella, pamoja Katibu Tawala wa mkoa huo kuanzia leo.

Rais Dkt. Magufuli ametengua uteuzi huo kutokana na mkoa huo kutajwa hauna wafanyakazi hewa, na tume iliyoundwa kufuatilia kubaini kuwa mkoa huo una wafanyakazi hewa 45.