Mtu mmoja aokotwa akiwa amefariki huko maeneo ya  Mombasa (Mbuyu mnene) Wilaya ya Mjini Unguja

Mwandishi wa Zanzibar24 amefanikiwa kufika kwenye tukio hilo na kuzungumza na baadhi ya mashuhuda ambae mmoja wapo ni Diwani wa wadi ya Mombasa Maulidi Mwinyi Mzee amesema maiti hiyo ni ya mwanamke na haitambulikali sababu ya kifochake isipokuwa karibu yake  kulikuwa na chupa za ulevi.

Hadi sasa maiti hiyo ipo mikononi mwa Askari Polisi kwakuendelea na utaratibu wa uchunguzi