Watu saba wanasadikiwa kupoteza maisha na wengine watatu kujeruhiwa kufuatia ajali ya gari la Azam Tv iliyotokea asubuhi hii Jumatatu Julai 8-2019 katika eneo la Malendi wilayani Iramba mkoani Singida.


Taarifa za awali zinaeleza kuwa gari Hilo lilikuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Chato.


Mganga mfawidhi wa hospitali ya Igunga Merichad Magongo amethibitisha kupokea majeruhi watatu katika hospitali ya Igunga.