Ofisa Habari wa Simba SC Haji Manara amemuonya Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera kukaa karibu na Wakongo ili kuwapa mbinu kuelekea mechi ya Simba dhidi ya AS Vita.

Manara ameeleza kuwa Kocha huyo amekuwa akizunguka na Vita jijini Dar es Salaam bila kujua kama anapaswa kuwa na majukumu ya kuisaidia timu yake ambayo ina mechi na Lipuli Jumamosi hii huko Iringa.

Ofisa huyo amemuonya Zahera kuwa makini na anachokifanya kwa sababu hii ni mechi ya kimataifa na kitaifa.

Amesema kuwa hii ni mechi ambayo nchi inajua, Rais anajua, sasa ole wake aendelee kuwaharibia mipango.