Haji Manara akamatwa na polisi, kutekwa Mo Dewji

Haji Manara amabae ni Ofisa Habari wa Simba, amekamatwa na polisi kutokana na tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’.

Manara alikamatwa jana jioni na kuachiwa kabla asubuhi ya Oktoba 12, 2018 kukamatwa tena na polisi.

Polisi waeleza mwanzo mwisho utekaji wa bilionea Mo Dewji

Akithibitisha kukamatwa kwa Manara, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema Manara anashikiliwa kutokana na kusambaza taarifa za tukio hilo kwenye mitandao ya kijamii kwa madai ya kutumwa na familia, jambo ambalo si kweli.

“Manara tunamshikilia kwa uchunguzi zaidi yeye amekuwa akisambaza taarifa mbalimbali za tukio hili kwenye mitandao ya kijamii kwa madai kuwa ametumwa na familia, lakini sio kweli, hajatumwa na familia hivyo tunamshikilia,” amesema Kamanda Mambosasa.

Mapema jana Manara alinukuliwa  akisema taarifa ya Mo kupata matatizo imemshtua kila mmoja na kwamba bado wanaliachia jeshi la polisi kufanya kazi ya kumpata mwekezaji wao.

“Wanasimba wawe watulivu wakiliachia jeshi la polisi kufanya kazi yake na kwamba wanaamini MO atapatikana akiwa hai,” alisema Manara.

Source: Mwananchi