Msemaji wa Klabu ya Simba Haji Manara amesema iwapo Simba watakuwa Mabigwa wa soka Afrika ataimaliza dunia yake salama kwa kurudi kijijini  na kujikita katika Shughuli nyengine za kijamii.

Haji Manara kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema “Simba ikiwa na Uwanja wake na vitegauchumi vyake lakini kubwa tuwe Mabingwa wa Afrika…..next ?kufanya kazi za kijamii iwe siasa au vinginevyo na kisha kuhamia kijijini kulima na kusomesha dini”