Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara, amethibitisha kupima virusi vya ugonjwa wa corona ambapo amebainisha kwamba,hana maambukizi ya virusi hivyo na yupo fiti ila bado hajaridhika anataka kupima tena afikapo Tanzania.

Manara ametoa taarifa hiyo baada ya kuwepo na wasiwasi kama atakuwa na virusi vya ugonjwa huo kwa sababu yupo nje ya nchi kwa muda mrefu na ametembelea nchi kama Hispania, Ufaransa, Canada na Uholanzi.

Wazungu baada ya kunipima Corona wakaniruhusu kupanda ndege yao, kisha kuniletea ubwabwa na mandondo na nikirudi home nitapima tena, bado nitaweka karantini ili nijiridhishe kama nipo fiti” ameandika Manara.

Aidha ameongeza kuandika “Ingawa hadi sasa Alhamdulillah nipo fiti kuliko chuma, ngoja nipige kubwa moja kisha nije kitaani Bongo”