Hali si hali: Gari za Abiria kizungumkuti Unguja

Ujenzi unaoendelea  nchini Zanzibar wa miundombinu ya barabara na mitaro umechangia   kupungua kwa huduma za usafirisha na kupelekea wananchi wa Zanzibar kupata usumbufu mkubwa wa usafiri.

Barabara mbalimbali zinazoendelea kujengwa na serikali ili kuondoa kero kwa madereva na wananchi wanazozitumia barabara hizo ikiwemo Bububu Mkokotoni,Fuoni kwerekwe,Mikunguni kwa Abass Hussein na Chukwani kiembe samaki zimechangia kupungua kwa ruti za magari ya abiria na nyengine kutolewa ruti na wamiliki wa magari hayo ili kupisha ujenzi kukamilika ambapo hali hiyo imechangia kuleta uhaba wa usafiri kwa wananchi.

Inafahamika kuwa maendeleo hayaji kwa urahisi katika nchi na ndio maana serikali ya Mapinduzi Zanzibar inapambana kuhakikisha inaweka miundombinu  rafiki ya barabara  kwa wananchi wote ili nchi ifikie kwenye maendeleo.

Baadhi ya wananchi wa viunga vya mjini na nje ya mji wametoa maoni yao akiwemo Halima Ali Haji mkaazi wa Chukwani Bakari Othman mkaazi wa Kwanyanya na wengi kwa nyakati tofauti wamesema kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la wananchi wanaohitaji usafiri wa umma hali hii imetokana na upungufu wa madaladala  uliochangiwa na utegenezwaji wa barabara hizo.

Wamesema wanashangazwa na upungufu huo wa magari ya abiria iliyojitokeza hali inayowapa wakati mgumu wananchi hasa wagonjwa na makundi maalum ya watu wenye ulemavu kushindwa kumudu fujo za  gari zilizopo  kwani zimekuwa zikijaza sana hadi kufikia watu kupigana  kwenye vituo vya daladala kutokana na kugombania usafiri ambao ni mchache na haukidhi haja.

Aidha wamesema usafiri unakuwa wa tabu nyakati za mchana, jioni hadi usiku huku  ongezeko la abiria kuwa kubwa huku  wanafunzi nao wanasumbuka na kupelekea kurudi majumbani  usiku muda wote wanaupoteza  katika vituo vya daladala.

Kwaupande wao baadhi ya Madereva wa daladala za Bububu Mjini,Kwerekwe,Chukwani,Nungwi na Mkokotoni wamesema  baadhi ya wamiliki wa gari hizo wameamua kuzihamisha ruti gari zao ili kupisha ujenzi wa barabara  kwani kuendeleo kuziwacha gari kufanyakazi ya kubeba abiri  nikuitia gari ubovu  kutokana na  mizunguko kuwa mingi huku nauli iliyowekwa ni ndogo mia 300 kwa gari za mjini na gari za shamba 1000 ambayo haikidhi.

Wamesema  kama serikali itaweza wawaengezee bei za nauli  ili waweze kumudu harama za mafuta pamoja na kuipa uhai gari kwani gari nyengi  hivi sasa zimekuwa chakavu zilizotokana na ubovu wa barabara.

Hata hivyo wamewataka wananchi kuwa wavumilivu pindi hichi ili kupisha ujenzi  huo kwani wao hawawezi  kuziacha gari kufanyakazi  huku kila siku spana mkononi.

“ kipindi hichi madereva wengi tunaumia  kutokana na kukosa ajira huku familia zikiwategemea” wamesema.

Hivyo madereva na abiria wametoa wito kwa serikali pamoja na idara husika za ujenzi wa barabara kuharakisha  ujenzi  huo wa barabara ili wananchi waweze kuondokana na usumbufu huo uliojitokeza kisiwani unguja.

Wamesema  kukosekana kwa barabara kumechangia  kusimama  kwa shughuli za uzalishaji na usafirishaji  kwa wananchi wa mjini na vijijini hasa  kwa wafanyabiashara wanashindwa kufanyakazi zao  hivyo hupelekea uchumi kwa wananchi kupungua.

Amina Omar