Wasanii wawili kutoka WCB, Harmonize na Rayvanny wametangaza kuachia kolabo yao ya kwanza iitwayo Paranawe leo 1:00 Jioni.

Harmonize kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema kuwa PARANAWE ndio itakuwa kolabo yake ya kufungia mwaka 2018.

Harmonize amewaomba BASATA na watalaam wa lugha kumsaidia maana halisi ya neno  PARANAWE ambalo amelitumia kama jina la wimbo huo.

Kwa mujibu wa Kamusi ya MACMILLAN neno Paranawe ni  neo la Kireno na lina maana ya ‘Mtu pekee shujaa/hodari au mwenye nguvu’.