Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), imetoa siku 7 kwa kamati ya Usalama na Maadili ya chama hicho kukamilisha taarifa ya mahojiano juu ya wanachama watatu, Yusuph Makamba, Abdulrahman Kinana na Bernard Membe na kuiwasilisha katika vikao husika.

Kikao cha kamati kuu kilichotoa maelekezo hayo kilifanyika Jana katika Ofisi ndogo za CCM Lumumba Dar es Salaam na kiliongozwa na Mwentekiti wa CCM Taifa Dkt John Pombe Magufuli.