Maneno ya mwisho aliyomwambia mama yake Yared Tessema Getachew “Narudi nyumbani Nairobi, nimeshau simu yangu hotelini, tutaongea zaidi nikifika huko”.

Rubani huyo kijana aliyekuwa akirusha ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia, iliyopata ajali mwishoni mwa wiki iliyopita na kuua watu 157 waliokuwemo

Maneno hayo alimwambia mama yake mzazi kwa kumtumia ujumbe wa simu, kabla ya kurusha ndege hiyo ya Boeing 737 Max 8, asubuhi ya Jumapili ya Machi 10, 2019.

Yared mwenye miaka 29 alikuwa ni raia wa Kenya, ndiye aliyekuwa rubani mkuu kwenye ndege hiyo iliyosababisha vifo vya mamia ya watu.

Mpaka sasa mwili wa rubani huyo bado haujapatikana, ili kufanyiwa mazishi kwa imani yake ya dini ya kiislam.