Haya ndio malengo ya serikali ya wanafunzi ndani ya skuli

Serikali za wanafunzi zimekuwa kiungo muhimu baina ya walimu na Wanafunzi ili kuleta mandeleo ya skuli zao .

Akizugumza na Zanzibar24 mwalimu mkuu wa Skuli ya AL HISAN GIRLS SECONDARY SCHOOL iliyopo Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharib B mwalimu Abdalla Nassor kwenye uchaguzi wa skuli hiyo amesema Serikali ya Wanafunzi imekuwa chachu kubwa ya  maendeleo ndani ya skuli yake kwa muda mrefu.

mwalimu mkuu wa Skuli ya AL HISAN GIRLS SECONDARY SCHOOL iliyopo Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharib B mwalimu Abdalla Nassor

Aidha amesema lengo la chaguzi hizo ni kuwajenga wigo wa Demokrasia  kwa vitendo wanafunzi ili kutanua maendeleo ya Elimu ya Siasa kwa maendeleo ya baadae ya nchi .

‘’Tunawafundisha Demokrasia kwa vitendo badala ya ile ya kusoma darasani sasa hapa tunawafundisha kwa vitendo miaka ya nyuma tulikuwa tukifanya chaguzi za kawaida ila kwa sasa tunafanya kama vile chaguzi za nchi tunapanga foleni na kuchagua viongozi wetu wa skuli’’ Alisema Mwalim Abdalla Nassor.

Kwa upande wake Raisi mstaafu wa skuli hiyo Zuwena Fadhil amesema kwenye mwaka wake uliopita wa uongozi ilikuwa chachu kubwa ya maendeleo ya skuli hiyo ikiwemo kuhamasisha usomaji wa somo la hesabu,kuanzishwa klabu za maendeleo na kujengwa kiwanja maalum cha michezo ndani ya skuli hiyo.

Mastura Saidi Khamisi ameibuka kuwa mshindi wa Uraisi ndani ya Skili hiyo ya Al Hisaan baada ya kupata jumla ya kura 360 dhidi ya mwanafunzi mwenziwe Weje Maalim Salehe aliepata kura 68 wote wa kidato cha Tano.