H

Waziri mkuu wa zamani wa New Zealand, Helen Clark ametangaza kuwania nafasi ya kuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Katika mahojiano na BBC amesema atalifanyia mabadiliko baraza la usalama la umoja wa mataifa kwa kuifanya Ujerumani,Japan,India na Brazil kuwa wanachama wa kudumu wa baraza la usalama la umoja wa mataifa.

Amesema pia nchi mbili za Afrika zinaweza kuwa wanachama wa kudumu kwa kutazama uhalisia katika karne ya 21.

Bi Clark kwa sasa ni mkuu wa Mpango wa maendeleo ndani ya umoja wa mataifa.

Amesema ana uzoefu usio na shaka kiasi cha kumuwezesha kumrithi Ban Ki-moon, ambaye anastaafu mwezi Desemba. Amesema Umoja wa mataifa unahitaji mikakati mipya ili kushughulikia masuala ya sasa ya amani na masuala ya usalama.

Wanawake wengine watatu wanawania nafasi ya mwanamke wa kwanza katibu Mkuu ndani ya UN. Wanaume wanne pia wanawania nafasi hiyo.

Mwanamama huyu aliongea na shirika la habari la Ufaransa, AFP akisema kuwa ana uzoefu wa zaidi ya miaka 30 nchini New Zealand na UN.

Wanaowania nafasi hiyo ni pamoja na Mkuu wa Unesco, Irina Bokova wa Bulgaria na Kamishna mkuu wa shirika la wakimbizi, Antonio Guterres wa Ureno.