Hii hapa Bei ya Mafuta Zanzibar kuanzia August 7, 2018

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma Nishati na Maji Zanzibar (ZURA) imetoa taarifa juu ya bei mpya za mafuta zitakazoanza rasmin kutumika kuanzia siku ya Jumanne ya tarehe 7-8-2018.

Hayo ameyasema huko ofisini kwake Maisara Kaimu Mkuu wa Kitengo cha uhusiano Khuzaimat Bakar Kheir kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu  wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya mabadiliko ya bei za mafuta ambayo yatakayoanza kesho.

Alisema mamlaka hiyo ya ZURA inakuwa na kawaida ya kupanga bei kwa kuzingatia mambo muhimu yafuatayo ikiwemo Wastani wa mwenendo wa mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la Dunia (Platts Quatations ) katika mwezi wa Juni , 2018 , kwa lengo la kupata kianzio cha kufanya mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Agosti , 2018.

Pia alisema Gharama za uingizaji na uhifadhi katika Bandari ya Dar es salaam  pamoja na gharama za kuyasafirisha tena hadi Zanzibar , gharama za usafiri , Bima na ‘Premium ‘ hadi Zanzibar , thamani ya shilingi ya Tanzania Dola , kodi za Serikali  na kiwango cha faida kwa wauzaji wa Jumla na Reja Reja.

Kaimu huyo alisema sababu za mabadiliko ya bei kwa bidhaa ya mafuta ni bei za bidhaa zote za  mafuta zimebadilika kwa wastani wa uuzaji wa bidhaa hizo katika soko la Dunia . Bei ya Mafuta ya Petroli katika soko  hilo la Dunia kwa Mwezi wa Julai , 2018 imeshuka kwa TSH . 13 sawa na asilimia 1% , bei ya mafuta ya Dizeli katika soko hili hilo la Dunia imeshuka kwa TSH . 33 sawa na asilimia 2.5% , bei ya mafuta ya Taa katika soko la Dunia imepanda kwa TSH . 107 sawa na asilimia 9% na Mafuta ya Banka imeshuka kwa TSH . 33 sawa na asilimia 2.5%.

Aidha alisema Gharama za Usafirishaji , Bima   na Premium ya Mafuta ya Petrol kwa Mwezi wa Julai , 2018 imeshuka kwa TSH .10 sawa na asilimia 0.6% . mafuta ya Dizeli imeshuka kwa Tsh . 3 sawa na asilimia 0.06% , Mafutaya Taa imepanda kwa TSH .18 sawa na asilimia 0.25% na Mafuta ya Banka imeshuka kwa TSH. 3 sawa na asilimia 0.06%.

Vile vile Gharama za bandari ya Dar es salaam hasa”Demurrage charges “ katika mwezi wa Julai , 2018 zimeshuka ikilinganishwa na mwezi wa Juni 2018, Petroli imeshuka kwa TSH . 1, kutoka TSH 6.97 kwa lita hadi TSH .6.14. Dizeli imeshuka kwa TSH. 1 kutokaTSH, 7.56 kwa lita hadi Tsh 6.65 na mafuta ya Taa imeshuka kwa TSH 9 kwa lita kutoka TSH 14.94 kwa Mwezi wa Juni , 2018 , hadi 5.58.

Alisema bei ya reje reja ya mafuta ya Petroli kwa mwezi wa Agosti , 2018 imeshuka kwa Shilingi 25 kwa lita kutoka Shilingi 2,435 ya mwezi hadi Julai , 2018 hadi Shilingi 2,410 kwa lita katika Mwezi wa Agosti , sawa na asilimia 1%.

Khuzaimat alisema bei ya reja reja ya  mafuta ya Dizeli kwa Mwezi wa Agosti , 2018 imeshuka kwa Shilingi 35 kwa lita kutoka Shilingi 2,430 ya mwezi wa Julai , 2018 hadi Shilingi 2,395 sawa na asilimia 1.4%.

Akiendelea kutoa bei za bidhaa hizo alisema bei ya reja reja ya Mafuta ya Taa kwa mwezi wa Agosti , 2018 imepanda kwa Shilingi 77 kwa lita kutoka Shilingi 1,777 kwa lita ya Mwezi wa Julai , 2018 hadi Shilingi 1,854 katika mwezi wa Agosti , 2018 sawa na asilimia 4%.

Sambamba na hayo  bei ya reja reja  ya mafuta ya Banka (Mafuta ya Meli ) kwa mwezi wa Agosti 2018. imeshuka kwa Shilingi 36 kwa lita kutoka Shilingi 2,259  kwa lita katika mwezi wa Julai, 2018hadi Shilingi 2,222 katika mwezi wa Agosti , 2018,  sawa na asilimia 1.5%.

Na pia bei ya reja reja ya Mafuta ya Ndege kwa mwezi wa Agosti , 2018 imeshuka kwa TSH 20.96  kwa lita kutoka TSH .1,936.73 kwa lita katika Mwezi wa Julai , 2018 hadi TSH . 1,915.77 katika mwezi wa Julai, 2018 sawa na asilimia 1%.