Kama wewe ni mmoja kati ya mashabiki wa malkia wa filamu Wema Sepetu, basi habari njema ni kwamba tiketi za ‘Birthday Gala’ zitaanza kuuzwa rasmi kuanzia kesho (Jumamosi) huku bei elekezi zikiwa ni 50000 kwa tiketi moja na kwa meza ya watu 10 ikiwa ni tsh 500,000.

Mrembo huyo atafanya matukio mawili kwa pamoja, uzinduzi wa filamu yake mpya ‘Dad’ alioshirikiana na Van Vicker kutoka Nigeria pamoja na kusherekea birthday yake ambayo ameiita Bithday Gala.

“Tarehe 15 tunatangaza Cards zitakapokuwa zinauzwa,” Wema Sepetu aliandika kupitia mtandao wake wa Instagram.

Katika ujumbe mwingine aliandika, “Wow…!!! Two weeks to Go… Nikimaanisha 14 Days… Haiya kazi ya Card kesho inaanza Inshallah… Zipo Chache sana… Zitakapokuwa SOLD OUT usilaumu mtu,”

Hili litakuwa ni tukio la kwanza la mrembo huyo toka ahukumiwe na Mahakama ya Kisutu baada ya kukutwa na hatia ya kutumia dawa za kulevya aina ya bangi.