Hii ndio sababu ya kusimamishwa Ligi daraja la kwanza kanda na daraja la piti Taifa kwa Unguja

Kamati ya Rufaa na Usuluhishi imezisimamisha kwa muda ligi Daraja la Kwanza Kanda na Ligi Daraja la Pili Taifa Unguja baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa timu ya Miembeni City ambayo imeitaka Kamati hiyo kuzisimamisha ligi hizo.

Akithibitisha kupokea Barua ya kusimamishwa ligi hizo Kaimu Katibu wa ZFA Khamis Abdallah Said amesema ZFA wamepokea Barua kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Rufaa na Usuluhishi Takky Abdulla Habib kwa kuzisimamisha ligi hizo kwa muda mpaka pale Kamati hiyo itakaposikiliza rufaa hiyo na kutoa maamuzi stahiki.

Aidha Khamisi Saidi amesema wao ZFA kupitia kamati hiyo ya rufaa na usulihishi wamejiridhisha kupitia malalamiko ya klabu ya MieMben City waliyoyatoa ya kushushwa daraja la pili Taifa msimu uliopita.

“Sisi kama ZFA kamati hii tumeunda yenyewe hivyo hatuna budi kuhakikisha tunaipa nafasi ya kufanya majukumu yake hivyo hakuna sababu haki za vilabu,haki za wachezaji zinafanyiwa kazi kupitia kamati ya rufaa na usuluhishi”.

‘’Tunaomba sana vilabu vitusamehe kwa hili vilikuwa vimesha jiandaa wale ambao wameshatumia gharama zao basi waandike ZFA tutalipa hizi gharama mpaka pale rufaa hii itapo sikilizwa basi ligi hizi zitandelea ’’ Alisema Khamisi Saidi.

Klabu ya Miemben City imegomea michezo mitatu ya ligi kuu ya Zanzibar msimu wa mwaka jana 2016/2017 baada ya kutumbuliwa rufaa yao dhidi ya klabu ya Chuoni na ZFA ikaamua kumshusha madaraja mawili kutoka Ligi kuu ya Zanzibar hadi ligi Daraja la pili Taifa.