Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema, Freeman Mbowe ametangaza chama hicho kutoshiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019 kwa madai kushiriki kwao ni kuhalalisha ubatili.

Maamuzi hayo ya Chama hicho kikuu cha upinzani hapa nchini yamefikiwa na wabunge wao waliokuwa leo Alasiri mjini Dodoma katika kikao cha kamati kuu ya dharura ya chama hicho.