Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetangaza kesi nyengine ya mgonjwa wa Corona. Mgonjwa huyo ni Mwanamke raia wa Ujerumani na ni mwenza wa mgonjwa wa kwanza ambae ni raia wa Ghana.

Kutokana na kesi hii Zanzibar imetimiza jumla ya kesi mbili za Ugonjwa wa Corona.