Aliyewahi kuwa Waziri katika Wizara mbalimbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Bw. Ramadhan Abdallah Shaaban amefariki Dunia.

Bw. Ramadhan Abdallah Shaaban aliyesimama enzi za uhai wake

Taarifa zilizotufikia ndani ya Chumba chetu cha Habari zinaeleza kuwa Bw. Shaaban amefariki Dunia katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam.

Ramadhan Abdallah Shaaban alikua Waziri wa Katiba na Utawala bora (2005 – 2010), Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali (2010 – 2012) na Waziri wa Ardhi Maji Nishati Nyumba na Makazi (2012 – 2015).