Baraza la Mitahani la Taifa (Necta) leo  Julai 11 2019  limetangaza rasmi matokeo ya kidato cha sita nchini ambapo ufaulu umeonekana kupanda ukilinganisha na mwaka wa jana.

Pamoja na matokeo kuwa mazuri sana kwa baadhi ya shule za mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, bado jinamizi la Shule za mkoa huo kuwa miongoni mwa shule 10 zilizofanya vibaya linaendelea kuundama mkoa huo.

Hizi hapa Shule 10 zilizofanya vibaya kwa mwaka huu

  1. Nyamunga kutoka mkoa wa Mara
  2. Haile Selassie kutoka mkoa wa Mjini Magharibi
  3. Tumekuja kutoka mkoa wa Mjini Magharibi
  4. Bumangi kutoka Mara
  5. Buturi kutoka Mara
  6. Mpendae kutoka Mjini Magharibi
  7. Eckernforde kutoka Tanga
  8. Nsimbo kutoka Katavi
  9. Mondo kutoka Dodoma
  10. Kiembe Samaki A Islamic kutoka mkoa wa Mjini Magharibi