Wananchi kisiwani pemba, wametakiwa kuhudhuria kwa wingi katika ufunguzi wa hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani inayo tarajiwa kufunguliwa rasmi tarehe 26 mwezi huu.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini pemba Mwanajuma Majidi Abdalla ,wakati alipokuwa akizungumza na  maafisa wadhamini wa wizara zote za serikali na watendaji wa tasisi nyegine hapo katika hospitali ya Abdalla Mzee mkoani Pemba.

Amesma kuwa lengo la kuitisha mkutano huo nikuzungumzia  maandalizi ya ufunguzi wa hospitali hiyo ambayo inatarajiwa kufunguliwa wiki ijahyo ya mwezi huu  ambapo mgeni rasmi katika  ufunguzi huo ni rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi dk Ali Muhammed Shein.

Nae Mkuu wa Wilaya Mkoani, nd Hemed Suleiman Abdalla, ameipongeza serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwajengea wananchi wake hospitali  ya rufaa kisiwani pemba hivyo hapana budi wananchi hao kuhudhuria kwa wingi siku ya ufunguzi kwani ni jamba la historia kubwa na la kujivunia kupata kitu hicho kwao.

Hata hivyo amemuoba afisa mdhami wa shirika la umeme pemba kuhakikisha kipindi hiki cha matayarisho ya ufunguzi wa hospitali umeme uwepo muda wote pamoja na kuongeza bidii za kukamilisha ukarabati wao ili kuweza kupata umeme wa uhakika .

Kwa upande wake mkurugenzi wa wizara afya Zanzibar Mohd Dahoma amesema kwamba maandalizi yako hatua mzuri hivyo amewahimiza wananchi kuungana nao ili kuona wanasherehekea ufunguzi huo wa hospitali hiyo mpya ya kisasa.