Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kuwa Hospitali ya Apollo India huenda ikasitisha kupokea wagonjwa kutoka nchini Tanzania  kutokana na deni kubwa inayodai.

Ameyasema hayo leo wakati alipokuwa akizindua bodi ya Wadhamini wa Taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI). Waziri Ummy amesema Hospiatali hiyo ya Apollo inaidai Tanzania kiasi cha shilingi Bilioni 30.

Kutokana na tishio hilo, Waziri Ummy amesema  kwamba wameshaanza kulipa deni hilo na jitihada kubwa zinfanywa ili kuweza kumalizia kabisa deni hilo ili wagonjwa waendelee kupokelewa na kutibiwa.