Jumla ya watahiniwa 88,069 sawa na asilimia 98.32 ya watahiniwa waliofanya mtihani kwa Tanzania nzima wamefaulu.  Wasichana waliofaulu ni 37,219 sawa na asilimia 99.11 wakati wavulana waliofaulu ni 50,850 sawa na asilimia 97.75. Kwa ujumla, asilimia ya ufaulu imeongezeka kwa asilimia 0.74.

 Kwa upande wa Skuli za Zanzibar, watahiniwa 2000 sawa na asilimia 96.85 ya watahiniwa wote wa skuli wamefaulu; kati yao  wasichana waliofaulu ni 1012 sawa na asilimia 49.01 na wavulana ni 988 sawa na asilimia 47.85.

Na kwa upande wa Zanzibar watahiniwa 1,837 sawa na asilimia 88.96 wamefaulu katika Daraja la I hadi III.

Takwimu za ufaulu kwa watahiniwa wa shule zinaonesha kuwa ufaulu katika masomo ya Geography, Kiswahili, English language, French Language, Arabic Language, Physcis, Chemistry, Agriculture, Computer Science, Basic Applied Mathemetics, Advanced Mathemetics, Economics, Commerce na Food and Human Nutrition umepanda ikilinganishwa na mwaka 2018.

Aidha, ufaulu katika masomo ya General Studies, History, Biology na Accountancy umeshuka kidogo ukilinganishwa na mwaka 2018.

Kwa ujumla matokeo ya mwaka 2019 kidato cha sita ni mazuri na yanaridhirisha. Hii inatokana na kuongezeka kwa ufaulu wa daraja la kwanza na pili.

Hatahivyo kwa matokeo hayo jumla ya wanafunzi 1,837 wana uwezo wa kujiunga na vyuo vikuu mbalimbali ndani na nje ya nchi. Pia wanafunzi 163 wanauwezo wa kujiunga na vyuo kwa ngazi ya stashahada.

Sambamba na hayo Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali inachukua fursa hiyo kuwapongeza wanafunzi, walimu na wazazi wote kwa mashirikiano mazuri waliyoonesha wakati wote.