Mshambuliaji wa Yanga Ibrahim Ajibu ameendelea kuwatetemesha mashabiki na wanachama wa timu hiyo kutokana na kuendelea kutokuwa sehemu ya kikosi cha timu.

Leo asubuhi Yanga imeondoka jijini Dar es Salaam kuelekea Morogoro kwa ajili ya mechi ya ligi dhidi ya Mtibwa Sugar bila yeye kuwepo.

Taarifa zilizo ndani ya Yanga zinasema Ajibu amekuwa akigomea kucheza akishinikiza mkataba mpya lakini uongozi umekuwa ukisema ni majeruhi.

Ni takribani inaenda wiki ya nne sasa Ajibu hajaichezea Yanga ambayo inahaha kupigania ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Mbali na Ajibu, beki Abdallah Shaibu Ninja naye hatakuwa sehemu ya mchezo kutokana na adhabu ya kufungiwa mechi tatu na TFF.