Wanafunzi wawili wa shule ya msingi Bwawani, Mtoni Kijichi Wilayani Temeke, wamefariki na wengine watatu kujeruhiwa baada ya kuangukiwa na ukuta wa uzio wa shule wakiwa wamekaa wakiendelea na shughuli zao za kawaida.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Polisi wa Temeke, Andrew Masatya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema limetokea leo asubuhi Desemba 6, 2018.

”Ni kweli wanafunzi wawili wamefariki, na wengine watatu wamejeruhiwa. Mmoja alifariki wakati wanakimbizwa Hospitali na mwingine amefariki akiwa hospitali tayari”, amesema Kamanda.

Aidha ameongeza majeruhi watatu wanaendelea vizuri, wakipatiwa huduma katika hospitali ya wilaya ya Temeke.