Watu watatu raia wa Tanzania wanashikiliwa na idara ya uhamiaji kwa tuhuma zakumiliki nyaraka bandia.

Akizungumza na Waandishi wa habari huko ofisini  kwake Kamishna Msaidizi wa idara hiyo ambae pia ni Mkuu wa kitengo cha sheria Kagimro Huseea  amesema watuhumiwa hao ni Halima Mohd Hassan, Miza Abdalla na Eric Julius Masanja walikamatwa tarehe 8/3/2019 majira ya Saa nane usiku  wakati idara ya uhamiaji ikiwa katika utekelezaji wa majukumu yake ya kazi .

Miongoni mwa nyaraka hizo ni Pasipoti 11,fomu za maombi ya paspoti, fomu ya uhamiaji inayojazwa wakati wa kuondoka hapa nchini, fomu ya maombi ya visa, kadi za bima za afya, vyeti vya kumaliza masomo vya vyuo mbalimbali, hati za ndoa, vyeti vya kuzaliwa vitano,  kitambulisho cha mzanzibar,  kadi za ATM, lesseni za biashara, TN namba ya TRA pamoja na risiti za malipo ya serikali ambazo hazijajazwa  na vitu vyengine. 

Wakati huo huo ameleeza tukio la pili ambalo  Raia sita wa kigeni wamekamatwa kwa makosa mbalimbali ya kiuhamiaji ikiwemo kufanya kazi bila vibali, kuzidisha muda wa kuishi nchini kuendelea kuishi bila hadhi maalumu. 

Amesema raia hao 6 ambao watatu kutoka kenya, na wengine kutoka uingereza, urusi, na India. 

Aisha kagimbo ametoa wito kwa wananchi kutoa mashirikiano kwa idara ya uhamiaji pindi  watakapobaini kuna mtu anaishi kinyume na sheria au watu wanaojihusisha na masuala ya uhalifu pamoja na kuhushi  nyaraka  za serikali na binafsi waweze kutoa taarifa mapema. 

Amesema uhamiaji inajukumu la kudhibiti uingiaji na utoaji wa wageni ambao hawapo nchini kisheria hivyo itaendele

Na:Amina Omar.