Jeshi la polisi linaendelea kumshikilia mchekeshaji maarufu Idris Sultan kwa sababu alijaribu kuharibu ushahidi na upelelezi umebaini alishiriki makosa mengine ya kimtandao.

Mchekeshaji huyo alikamatwa na kushikiliwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay Jijini Dar ambako alihojiwa kwa tuhuma za uonevu wa Kimtandao ikiwa ni siku chache baada ya kuweka picha ya zamani ya Rais Magufuli iliyoambatana na video yake akicheka

Msemaji wa Polisi, David Misime amesema “Tunaendelea kumshikilia kwasababu kubwa mbili; moja ni kuwa baada ya kutakiwa kuripoti Polisi alijaribu kuharibu ushahidi na pili ni katika upelelezi wetu tumebaini makosa mengine ya Kimtandao aliyokuwa akiyafanya”

Pia, ameongeza “Katika mahojiano tuliyofanya naye tulibaini alitumia namba ya simu isiyo yake katika kutenda uhalifu huo hivyo ushirikiano wake ndio utakaomfanya aendelee kukaa kituoni