Hii hapa video inayoonyesha askari watatu wa Kikosi cha Usalama Barabarani wakimshambulia dereva wa lori.

Katika video hiyo, askari wanaonekana wakimshambulia dereva huyu katika jitihada za kutaka kumkamata na kumdhibiti lakini alionekana kufanikiwa kujinasua katika mikono yao.


Katika patashika hiyo, dereva huyo anasikika akipiga kelele kuomba msaada akilalamika kung’atwa shingoni na mmoja wa askari.
Baada ya kufanikiwa kutoka katika mikono ya askari dereva wa lori alionekana kukimbilia katika gari na kuchukua panga jambo ambalo liliwafanya watu kutimua mbio.

Tukio hilo limeibua mjadala mkubwa katika mitandao ya kijamii kutokana na jinsi askari hao walivyotumia nguvu kubwa kumkamata dereva huyo ambaye haikufahamika mara kosa alilotendana alikokuwa akitokea au kuelekea.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe limesema litatoa tamko la tukio hilo haraka iwezekanavyo.

Angalia video hiyo hapo chini:

Chanzo: Mwananchi.