Binti aliyefiwa na wazazi wake wawili na ndugu zake watatu waliopata ajali wakati wakienda kwenye mahafali yake mkoani Kilimanjaro Oktoba 26, 2019 leo Jumamosi Novemba 16, 2019 amefahamishwa kuhusu vifo hivyo.

Amewasili nyumbani kwao Goba  Dar es Salaam alfajiri akitokea shule ya Sekondari ya Mather Theresia of Calcuta baada ya kumaliza mtihani wa Taifa wa kidato cha nne ulioanza Novemba 4, 2019.

Wazazi wake,  Lingston Zambi na Winifrida Lyimo na wadogo zake watatu, Lulu, Andrew na Grace walikufa katika ajali hiyo baada ya gari walilokuwa kusombwa na maji kutokana na mvua kubwa iliyonyesha wilayani Handeni mkoani Tanga.

Baada ya vifo hivyo, Anna ambaye hakuelezwa chochote na hata alipomaliza mitihani yake pia hakuambiwa mpaka leo alipofika nyumbani na kupewa habari hizo.

Ndugu zake walipata wakati mgumu kuhusu jinsi ya kuanza kumpa taarifa hiyo ya huzuni.