Jamii mkoani kagera imetakiwa kuondokana na dhana juu ya watoto wao wa kike wanaojitosa katika kinyang’anyiro cha kuwania taji la urembo.

Kauli hiyo ilitolewa na muandaaji wa Miss kagera mwaka huu Bi Violet Guntram Liganga katika zoezi la kusaka vipaji kwa warembo hao kabla ya kumtafuta mshindi wa kutwaa taji hilo zoezi litakalofanyika June 30 mwaka huku.

Bi Guntram amesema kuwa amekumbana na changamoto katika zoezi hilo kutokana na uelewa mdogo wa wazazi na jamii nzima kudai kuwa kuwania umiss ni jambo la UHUNI” kutokana na kauli hiyo alisema kuwa kama kauli mbiu ya mwaka huu inavyosema kuwa urembo ni heshima jamii inatakiwa kuondokana na dhana hiyo kwani ukipata taji hilo faida zake ni nyingi ikiwemo, kipato, Elimu ya kijinsia , jinsi ya kuishi vizuri na jamii ,kubadili tabia na mienendo mibovu.

Mwandaaji huyo alisema mashindano hayo yamekwama takribani miaka 2 mkoani kagera kutokana na dhana hiyo ambayo imewakatisha tamaa