Kaimu Kamanda wa  Polisi  Kikosi Cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mjini Magharibi Inspecta Jabir Hassan amewataka madereva wa vyombo vya moto kuheshimu alama za barabaran zilizowekwa ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.

Akizungumza na Zanzibar24 huko ofisini kwake Madema Inspecta Jabir amesema alama za Zebra Cross zinazowekwa katika maeneo maalum ikiwemo hospitalini ,sokoni pamoja na mashuleni zinasaidia kuepusha ajali kwa waendao kwa miguu hivyo ni wajibu wa madereva wote kuzingatia hilo ili kunusuru vifo vya watu na wengine kupata ulemavu wa kudumu.
Amesema madereva wanapaswa kuangalia  kwa makini kushoto na kulia na kuendesha vyombo vyao vya moto kwa Speed 20  badala ya  speed 50 wakati wanapokatiza katika alama hiyo.
Aidha Inspecta Jabir amewasihi madereva wawe waangalizi upande wa zebra cross kwa sababu maeneo hayo yanatumiwa na watu wengi wakiwemo walemavu hata watumiaji wa miguu na kuwataka kuheshimu zebra cross zilizowekwa katika barabara.
Rauhiya Mussa Shaaban